Mwanamuziki RICHARD FRANCIS NAMWATA TIMOTHEO a.k.a T Max,Mamamaamtiii a.k.a Mapafu ya mbwa hapo juzi ndipo aliwasili kwenye uwanja wa ndege mjini Bruxelles/Belgium ambapo alipokelewa na watu wengi wakiwemo vile vile mashabiki wake toka pande za Uholanzi ambao nawao waisubiri tarehe 7/July ambapo kombaini ya Warundi wanao ishi Ubelgigi watasheherekeya miaka 50 ya Uhuru wa Burundi.Hadi sasa kwenye horodha ya waimbaji watakao burudisha na kuelimisha watakao hudhuriya kwenye Tamasha hilo litakalo wakusanya waimbaji vigogo wa Burundi T Max mwenyewe ndo kishafika,na hapa leo au kesho wasubiriwa YOYA na UWINYOTA RIZIKI,na ifikapo hapo tarehe 6/July watakuwa tayari wamewasili AFRICA NOVA na DJ NICOLAS toka Canada,waimbaji kama Big Farious & Kidum wao wako tayari kule kwa jitihada yakupokeya wageni hao.Fahamu ya kuwa Tamasha hilo inaandaliwa na uwezo mkubwa,moja nikuonyesha Ulimwengu kuwa tunao waimbaji ambao wanao uwezo wakukonga nyoyo za watu kupitiya kazi nzuri ya production ya nyimbo zao wanazo imba.Kumbuka tena kuwa mwanamziki T Max alisafiri pamoja nae EXCELLENT NIMUBONA na Mkurugenzi mkuu kwenye Wizara ya Vijana na Tamaduni SINZINKAYO Léonard.Safari yao ilikwenda muruha,walifurahi na mapokezi ya warundi wanao ishi kule kama ABOUBAKAR,JEREMIE HAKESHIMANA,CYBILLE CISHAHAYO…
Alitwambiya MARTINE,raia Mrundi anae ishi Uhollanzi:“Nilishindwa kujikaza nilipo pata taarifa kuwa T MAX yupo kwenye horodha ya waimbaji watakao turusha roho hapo tarehe 7/July,nilitoka Uholanzi na ndugu zangu ili kwenda kuwapokea,ni furaha kubwa kwangu na kuona mwenyewe ametimiza ndoto yake aliyo kuwa nayo kujitangaza zaidi kimziki,siku hiyo moto utawaka siyo siri kwakua atakuwa pamoja na Mwanajeshi mwenzake Big Farious.”Tamasha hilo linamulikiwa kufanyika ifikapo hapo tarehe 7/July/2012 hapo hapo Bruxelles.Itaendeleya…
Aucun commentaire:
Enregistrer un commentaire