mardi 10 juillet 2012

Tamasha yakuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Burundi imefanyika hapo jana Bruxelles/Belgium…



T max,Chiba & Farious
Tamasha iliyo kuwa inasubiri kwa hamu Ulaya hususani kwa kombaini ya Warundi na Wanyarwanda sana sana wanao ishi kule ilifanyika hapo jana mjini Bruxelles,kwakuwa hatukuwa na ripota wetu kule tlijifunza tutumiye njiya ipi ili tupate hali halisi ya mambo yalivyo kuwa sehemu zile,ndo tukapata mmoja kati ya waimbaji wa hapa nchini Burundi ajulikane kwa jina la Ayubu a.k.a AB anae unda kundi nzima la Brothers Unit na akawa ametusimuliya haya yafwatayo

www.burundinyambo.blogspot.com
Nataka kukufahamisha kuwa Concert ya tarehe 7/July Bruxelles ili kuwa nzuri sana. Waimbaji wetu wameonesha uwezo mkubwa sana kitu ambacho kimefurahisha sana. Jana hata mimi nimeshuka Bruxelles kutokeya Ufaransa kwenda kuwaona waimbaji wenzangu wenye nimekuwa na muda mrefu kidogo siwaoni piya nimeweza kumuona Africa Nova ambaye nimekuwa sijawahi kuona face 2 face mbali na runinga ya RTNB.Kutokana na muda, kila muimbaji amepewa fursa ya kuimba nyimbo mbilimbili. T-Max amegusiya kidogo Bujumbura ndo nyumbani, Sanaa we umenitowa mbali…,akamaliziya Ndabaramutsa ambapo ukumbi wa watu umesimama nakuanza kucheza. Yoya ametuimbiya Uramumbwirira pamoja na wiyumva gute ambopo ameonesha uwezo mukubwa kwasababu imekuwa live ambapo ametufurahisha sana.”

Hassan Hossam & Yoya
Huyo ni Mrundi anaye ishi Ufaransa alijielekeza Belgium alitupa habari hiyo kwa muhtasari.Shukran sana…

 Yoya,Fariouz,T max

Aucun commentaire: