mardi 10 juillet 2012

Imuhira Festival haikwenda kama tulivyo fikiriya apo awali…



www.burundinyambo.blogspot.com
kama tulivyo wafahamisheni mwishoni mwa jumaa iliyopita Burundi ilikuwa imepata fursa yakuanda Festival yakimataifa iliyo zikutanisha nchi tofauti za kanda ya Afrika Mashariki na Jamuhuri yakidemokrasia ya Congo.Walikuwa wamesubiriwa wasanii vigogo barani Afrika kama Weasel & Redio toka Ouganda katika kundi la Good Life,Jaguar,Tom Close,Diamond,Docter Claude,Mickeal Ross na Papa Wemba.Kwa taarifa tulizo zipata toka kwa aliye kuwa anasimamiya mambo yakupasha habari Landry MUGISHA alitwambiya:“Ni mambo mengi yaliyo tuma Tamasha isifanyiki siku mbili apo nikizungumziya Jumaa-mosi na Jumaa-pili,mambo yaliyo sababisha pengine ifikapo hapo kesho ntaweza kuyaweka wazi kwani kuna mambo wako wanafatiliya Bank kwa upande wa mambo ya hesabu tuliyo yafanya na Kampuni kutoka Ouganda tuliyo ingiya nayo mkataba kuhusikana na swali nzima la ufundi(Sonorisation),ni mambo mengi yaliyo ingiliyana ndugu yangu na yakatuma Tamasha lisiendeki kama tulivyo kuwa tulitangaza kupitiya vituo tofauti vya Radio na Television,kwa kweli twa omba radhi kwa watu wote walio weza kutokeya siku zote hizo 4.Fahamu yakuwa Tamasha rasmi ilianza hapo tarehe 5/July/2012 kwenye ukumbi huyo huyo wa EFI tarafani NYAKABIGA,siku hiyo watu wengi wali itika wito na walikuwa wengi kweli,siku ya pili hapo tarehe 6/July/2012 watu walikuwa wengi vile vile,siku ya tatu hapo tarehe 7/July/2012 watu wali itika ila bahati mbaya hawakuburudika na muziki kama walivyokuwa wanasubiriya.Na hivo hivo jana hapakuwa lolote.tusubiri muelezo wawalio anda Tamasha hiyo ili tujuwe ni kipi kilicho sababisha kwani apo awali kama tulivyo wajulisheni Festival hiyo ingelichukuwa pengine na fasi ya kwanza kwa Tamasha zote zilizo kuwa zimeandaliwa nchini Burundi apo tukinukulu misemo ya LANDRY MUGISHA (chargé de la Communication).Itaendeleya…

Aucun commentaire: